Monday, October 31, 2011

MISS TANZANIA SEHEMU YA KWANZA

“Patrick amka basi darl inakaribia saa nne sasa”Alisema Veronika kwa sauti laini ya kubembeleza.
‘Mmmmhhh”Aliguna Patrick ,akajigeuza upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.
“Amka basi bwana uende ukaoge”Alizidi kubembeleza Veronika
Kwa uchovu mwingi Patrick akaamka na kunyoosha mikono yake juu huku akijipinda
“Loh !I’m veeery tired”Akasema kwa uchovu.
“lakini ukishaoga uchovu wote utaisha my darling “Akadakia Vero.
Kwa uvivu Patrick akajiinua kitandani na kuelekea bafuni .Dakika chache baadae alitoka akiwa amechangamka.
‘Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu.Sasa najisikia saafi kabisa.Nadhani itabidi kwa sasa nipunguze muda wa kufanya kazi .Nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi sana kwa siku kiasi kwamba nakosa hata muda wa kupumzika.naogopa  tukija kuonana nisije kuwa nashindwa kutimiza majukumu yangu kama mume kwa sababu ya uchovu”
Vero akatabasamu halafu akatoa kicheko cha chini chini na kusema
“Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kujaribu kupata muda wa kutosha wa kupumzika.”
“Nitajitahidi baby”
Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero akamshika mkono Patrick na kumpeleka sebuleni kupata stafstahi.
“Patrick dear nataka unisindikize Supermarket nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani .Si unajua kesho Andrew na vicktoria wameahidi kututembelea”Alisema Veronika wakati wakiendelea kupata chai.
“Mhh Vero we nenda tu mwenyewe mi niache nipumzike bwana”Patrick akajibu
“jamani dear usifanye hivyo naomba bwana unisindikize ,mi naona uvivu kwenda peke yangu”
‘haya mama ,tumalize twende ili tuwahi kurudi”
“Nashukuru dear”
Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa kuwa navyo ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi.
******************************************************************
Veronika Rugi alikuwa ni binti mrembo mwenye mvuto wa aina yake.Binti huyu licha ya kujaaliwa kichwa kizuri chenye nywele laini ,nyingi na ndefu ,alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionakshiwa na macho mapana yenye kurembua muda wote.Midomo mizuri ,laini ambayo akikupiga busu hutatamani abanduke.Mtoto huyu alijaaliwa shingo murua ambayo iliungana na kiwiliwili kilichokuwa na kifua chenye kupendeza kilichobeba chucu changa zenye kusisimua,zenye kuwatoa udenda wakware.Kimwana huyu mwenye uzuri usiopimika alijaaliwa umbo la utatanishi kuanzia kiunoni kushuka chini.Ni mabinti wachache sana waliopewa upendeleo wa namna hii na manani..
Pamoja na sifa hizo zote za nje lakini bado alikuwa na sifa lukuki za ndani.Kikubwa zaidi kinachomfanya apendwe na kila mtu ni uwezo wake mkubwa wa uelewa .Ni binti mwenye roho nzuri ya huruma na upendo asiyependa kujivuna wala kujikweza licha ya uwezo mkubwa familia yake ilionao.Ni binti mwenye heshima kwa watu wa rika zote ,mcheshi,asiyependa ubinafsi na zaidi ya yote ni mtu anayejua kupenda.
Veronika ambaye bado anaishi na mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka kadhaa iliyopita ,alikuwa ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ambayo haikubahatika kuwa na mtoto wa kiume.Dada mkubwa wa Veronika aliyeitwa Loniki hivi sasa anafanya kazi katika shirika la ndege la British airways ,ameolewa na anaishi nchini Uingereza.Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia hii ni ni binti mrembo sana Sarah ambaye aliwahi kushika nafasi ya tatu katika kinyan’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa.naye amekwishaolewa na ni afisa mahusiano wa benki moja mpya kabisa nchini iitwayo African meckat bank.Mtoto wa tatu na wa mwisho ni Veronika ambaye bado hajaolewa ,ila alikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mchumba wake Patrick.Ni hivi karibuni tu amehitimu shahada yake ya kwanza ya biashara katika chuo kikuu cha dar es salaam.Yeye ndiye msimamizi mkuu wa miradi yao yote ya familia kwa sasa.
******************************************************************
“basi nikwambie mpenzi nilisahau kukwambia toka mapema kuwa dada Loniki alifurahi sana kusikia kuwa tunataka tukafanye shopping ya harusi yetu nchini Uingrereza,nakwambia alifurahi huyo na akaahidi kuwa yeye na mumewe watagharamia safari nzima ya kwenda na kurudi na gharama zote za manunuzi.Amesisitiza kuwa tusitumie hata shilingi yetu.Kwa maana hiyo wiki hii nataka niende tena kufuatilia yale maombi yetu ya viza pale ubalozini.Nadhani kama Mungu akijaalia basi ndani ya wiki mbili zijazo tutakuwa tumeshakamilisha taratibu zote zinazotakiwa.”
Alisema Vero huku akijiegemeza karibu zaidi na kifua cha Patrick.Muda huo ilipata saa mbili za usiku na bado walikuwa wakipunga hewa safi baada ya mlo wa jioni.
“Wow! Hongera sana Vero kwa kuwa na ndugu wakarimu na wenye upendo wa hali ya juu sana kama ulivyo wewe.Tena umeongea kuhusu Loniki nimekumbuka na zile CD alizonitumia wiki iliyopita.Unajua sijatazama hata moja.Hebu twende ndani nikaitazame ile CD mpya ya Jack bauer.”
Alsema Patrick huku akijiinua toka pale walipokuwa wameketi na kuelekea sebuleni .Vero naye akakusanya vitu vyote vilivyokuwapo hapo chini naye akaingia ndani.
“Vero mbona ile CD ya Jack bauer  siioni hapa?au Andrew aliichukua?Aliuliza Patrick baada ya kuitafuta CD ile bila kuiona.
“Yawezekana Andrew atakuwa aliichukua kwa sababu siku ile aliing’ang;ania sana.Nakumbuka kuna CD alizichukua hapo nadhani na hiyo nayo ilikuwapo.”Akasema Vero
Patrick akalifunga kabati ,akaelekea katika friji akafungua na kujimimia Juice katika glasi .Vero alikuwa ameketi sofani akitazama Luninga.
“basi nakwambia Patrick ,Miss Tanzania ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa sana kwa sababu mabinti ni warembo kupita maelezo.Mhh………..”
Alisema Vero huku amekodoa macho yake katikaLuninga kubwa iliyokuwamo humo sebuleni.
“kwani fainali  za miss Tanzania ni lini?”Patrick akauliza
“Ni jumamosi ijayo na itafanyikia pale Diamond Jubilee.Kutapambwa na onyesho kali la machozi band,vile vile wana Fm academia na wasanii wengine kibao.Nataka kesho nikakate tiketi zetu za V.I P ili tusikose nafasi siku hiyo”Alisema Vero
Akiwa na juice yake mkononi Patrick akajisogeza taratibu kuelekea mahali alipokaa Veronika .kabl;a hajafika sofani alisimama akapiga funda la juice kisha akaelekeza macho yake katika luninga
“Naitwa Neema japhet ni mrembo toka kanda ya kaskazini.Ni miss Arusha.napendelea sana muziki wa dini,kusoma na michezo mbali mbali.Nategemea kuja kuwa mwanamitindo wa kimataifa.Iwapo nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitajikita zaidi katika kuwasaidia watoto yatima kwani naelewa mateso na machungu wanayaoyapata kwa kutokuwa na wazazi wao.Naombeni kura zenu namba yangu ya ushiriki ni ishirini.”Alikuwa ni mrembo wa Arusha akijinadi katika kipindi maalum cha kuwatambulisha washiriki wa kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kilichorushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa.
“Du! Si mchezo”Aliguna Patrick huku akisogelea zaidi Luninga
“nimekwambia Patrick warembo wa mwaka huu si mchezo .Hebu kaa uangalie jinsi watoto walivyobomba”Alisema Vero
“Naitwa Happy kibaho.Ni mrembo wa wilaya ya Ilala .Napendelea sana muziki laini,kusoma hadithi ,magazeti,kutazama luninga,na wanyama.nategemea kuwa mwanasheria.Iwapo nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitaelekeza nguvu zangu zote katika kuwasadia vijana wajasiria mali ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafadhili,nitaitumia kofia yangu kuiomba serikali ielekeze nguvu zake zaidi katika kuwasaidia vijana hawa katika kuwapatia mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha ili kupambana na ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira.Ninaomba kura zenu ili niweze kulitwaa taji hili la miss Tanzania kwani nina vigezo vyote vya kulitwaa taji hili .Namba yangu ya ushiriki ni 6.”
“Whaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!........................”Patrick Alipiga ukelele mkubwa
“Nooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!..I cant ……………………”alishindwa kuendelea glasi aliyoishika ikamponyoka na kuvunjika .Taratibu nguvu zikaanza kumwishia akadondokea sofani kisha akapoteza fahamu.
 “Patrick ,Patrick what’s wrong!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.........”
Alihamaki Veronika huku akimsogelea Patrick pale sofani na kumtingisha.
“Patrick darling what’s wrong with you?
Alizidi kuuliza Vero huku akimtingisha.
“Oooooh!Nooooooooooo!!!!!!!!Wake up Patriick”Alipiga ukelele baada ya kugundua kuwa Patrick hakuwa na fahamu.Vero akataharuki asijue afanye nini.hakukuwa na mtu yoyote wa karibu ambaye angeweza kumsaidia .Alitoka kutaka kwenda kuwaita majirani ,akafika mlangoni na kurudi tena ndani mpaka sofani alipolala Patrick.
“Patrick ,Patrick dear what’s wrong with you.Whats’s wrong Patrick!!!!!!!!!!!!!!”Vero aliongea peke yake huku machozi yakimtiririka.Pale pale akapata wazo la kumpeleka Patrick hospitali.Kwa nguvu zake zote akamuinua Patrick na kumpakia garini ,akakimbia kufungua geti kisha akaingia garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu pasina kufunga mlango wowote wa nyumba.

 Mpenzi msomaji endelea kufuatilia riwaya hii katika sehemu ijayo…….

No comments:

Post a Comment